(Yuda alinunua shamba kwa njia ya feza alizopata kwa ajili ya kitendo chake cha uovu. Pale akaangukia kichwa chini, maiti yakapasuka na matumbotumbo yake yote yakatoka inje.
Na kwa sababu ya tamaa yao mbaya ya mali, walimu hawa wa uongo watajipatia faida juu yenu kwa njia ya maneno ya uongo. Lakini tangia zamani hukumu yao imekwisha kutangazwa, nao hawatakawia kuangamizwa.
Ole kwao! Maana wamefuata njia ya Kaina. Kwa ajili ya kupata mali wameanguka katika kosa Balama alilofanya. Wameangamia kwa sababu wameasi kama vile Kora alivyoasi.