Mutawala huyo atafanya mapatano imara na watu wengi kwa muda wa miaka saba. Kisha nusu ya muda huo atakomesha sadaka za kuteketezwa kwa moto na sadaka zingine. Pahali pa juu katika hekalu patasimamishwa chukizo linaloleta uharibifu, nalo litabaki pale mpaka yule aliyemusimamisha atakapoangamizwa kama ilivyopangwa na Mungu.