Bwana wetu Yawe atakiangamiza kifo milele! Atayafuta machozi katika nyuso za watu wote na kuondoa haya ya watu wake katika dunia yote. Yawe amesema hivyo.
Inanipasa kuwakomboa hawa watu kutoka kuzimu; sharti niwaokoe kutoka kifo! Ewe kifo, mapigo yako ni wapi? Ewe kuzimu, kuangamiza kwako ni wapi? Mimi sitawaonea tena huruma!
Yawe wa majeshi anasema hivi: Ukifuata njia zangu na kushika maagizo niliyokupa, basi, utaisimamia nyumba yangu na viwanja vyake. Nami nitakuwezesha kuingia katika utumishi wangu kama hawa wanaosimama mbele yangu.
Itakuwa hivi vilevile wakati wafu watakapofufuka. Mwili unazikwa katika udongo katika hali ya kuharibika, lakini unapofufuka, unafufuka na hali ya kutoweza kuharibika
Yeye atabadilisha huu mwili wetu wa uzaifu na kuufananisha na mwili wake wa utukufu kwa nguvu ambayo kwa njia yake anaweza kuwa na mamlaka juu ya vitu vyote.
Heri na baraka sana kwa wale watakaokuwa katika ufufuko wa kwanza! Kifo cha pili hakina uwezo juu yao, nao watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, na watatawala pamoja naye kwa muda wa miaka elfu moja.
Lakini akaniambia: “Angalia, usifanye vile! Kwa maana mimi ni mutumishi kama vile wewe, na wandugu zako manabii na watu wanaoshika maneno ya unabii yanayoandikwa katika kitabu hiki. Ni Mungu ndiye unayepaswa kumwabudu!”