Luka 17:27 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
27 Siku zile watu walikuwa wakikula na kunywa, wakioa na kuolewa mpaka ilipotimia siku ile Noa alipoingia ndani ya chombo. Halafu mvua kubwa ikanyesha na kuwaangamiza wote.
Mungu akaangamiza kila kiumbe kilichokuwa na pumzi ya uzima katika dunia: wanadamu, nyama, viumbe vinavyotambaa na ndege wa anga. Vyote viliangamizwa katika dunia. Noa tu ndiye aliyebaki na wale waliokuwa pamoja naye ndani ya chombo.
Lakini hasara itakupata ambayo hautaweza kujiepusha nayo. Magumu yatakutokea ambayo hautaweza kuyapinga; maangamizi yatakufikia kwa rafla ambayo haujapata kuyaona hata kidogo.
Yule kijana alimwongoza Daudi mpaka kwenye kundi lile. Walipofika kule waliwakuta wanyanganyi wale wakiwa wametawanyika kila pahali maana walikuwa wakikula na kunywa kwa sababu vitu walivyonyanganya kutoka inchi ya Wafilistini na inchi ya Yuda vilikuwa vingi sana.