Kutoka 39:3 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
3 Wakafua zahabu na kuikata katika nyuzi nyembamba kwa kuzifuma pamoja na sufu ya rangi ya samawi, ya zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa kwa ufundi.
Zaidi ya hayo yote, utatengeneza hema takatifu kwa mapazia kumi ya kitani safi iliyosokotwa, na kwa sufu ya rangi ya samawi, zambarau na nyekundu. Mapazia hayo utayapamba kwa makerubi waliochorwa.
Wanaume wote wenye ujuzi wakatengeneza hema takatifu kwa mapazia kumi ya kitani safi iliyosokotwa, na kwa sufu ya rangi ya samawi, zambarau na nyekundu, na kuchora makerubi.