Chumba cha ndani, kilichoitwa Pahali Patakatifu Sana, kilijengwa katika sehemu ya nyuma ya nyumba. Kilikuwa kimejengwa kwa mbao za mierezi kutokea kwenye sakafu mpaka kwenye dari, na urefu wake ulikuwa metre tisa.
Kisha akatwaa vile vibao viwili vya mawe na kuviweka katika lile sanduku. Akapitisha ile miti katika vikomo vya sanduku na kuweka kiti cha rehema juu yake.
Akakipima chumba chenyewe, nacho kilikuwa cha muraba pande zake zikiwa na upana wa metre kumi. Chumba hiki kilikuwa mbele ya baraza la katikati. Kisha, akaniambia: Hapa ndipo Pahali Patakatifu Sana.
Akamwambia: Umwambie ndugu yako Haruni asiingie katika Pahali Patakatifu nyuma ya pazia wakati usiokubaliwa. Asiingie pahali pale maana ndipo nitakapotokea katika wingu juu ya kiti cha rehema. Asipotii, atakufa.
Na juu ya lile sanduku kulikuwa sanamu mbili za makerubi zilizoonyesha utukufu wa Mungu. Mabawa yao yalikuwa yakinyooshwa juu ya kiti cha rehema. Lakini sasa si wakati wa kueleza mambo hayo yote moja kwa moja.