Halafu, Musa akamwambia Mungu: “Sasa, nikiwaendea Waisraeli na kuwaambia: ‘Mungu wa babu zenu amenituma kwenu’, nao wakiniuliza: ‘Jina lake ni nani?’, nitawaambia nini?”
Uwaambie Waisraeli kwamba: Yawe, Mungu wa babu zenu, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo, amekutuma kwao. Hili ndilo jina langu milele, na hivi ndivyo nitakavyokumbukwa katika vizazi vyote.
Yawe anajitokeza kama shujaa; kama vile askari katika vita anatatanua kupigana. Anapiga kelele kubwa la vita na kujionyesha mwenye nguvu juu ya waadui zake.