Kisha alimwamuru Uria: “Tumia hii mazabahu yangu kubwa kwa kuteketeza sadaka za asubui na sadaka za unga za magaribi, sadaka za kuteketezwa, sadaka za unga za mufalme na za watu wote na vilevile sadaka za divai za watu. Unyunyize damu ya nyama wote wa kuteketezwa ambao wametolewa sadaka. Lakini ile mazabahu ya shaba nitaitumia mimi kwa kuuliza shauri toka kwa Mungu.”