Wafalme watakushugulikia, na malkia watakutengenezea chakula. Watainama mbele yako uso mpaka chini, na kulambula mavumbi ya miguu yako. Halafu utatambua kwamba mimi ni Yawe; wote wanaonitegemea hawatapata haya.
Utaletewa chakula na watu wa mataifa; wafalme watakupatia chakula bora. Hapo utatambua kwamba mimi Yawe ni Mwokozi wako; mimi Mwenye Nguvu wa Yakobo ni Mukombozi wako.
Halafu utaona na utafurahi, moyo wako utasisimuka na kushangilia. Maana utajiri tokea ngambo ya bahari utakufikia kwa wingi, mali za mataifa zitaletwa kwako.