Litachanua maua kwa wingi kama waridi, litashangilia na kuimba kwa furaha. Mungu atalijalia utukufu wa milima ya Lebanoni, uzuri wa mulima Karmeli na wa bonde la Saroni. Watu watauona utukufu wa Yawe, watauona ukubwa wa Mungu wetu.
Yawe wa majeshi anasema hivi: Pahali hapa ambapo ni jangwa bila watu wala nyama, na katika miji yake yote, patakuwa shamba ambalo wachungaji watakulisha ndani yake makundi yao ya kondoo.
Nitawarudisha Waisraeli katika inchi yao, nao watakula mavuno yatakayolimwa juu ya mulima Karmeli na Basani na watatosheka kwa chakula kutoka milima ya Efuraimu na Gileadi.
Nitamulipiza kwa ajili ya siku alizoabudu sanamu za mungu Bali, kwa ajili ya muda alioutumia kuzifukizia ubani, akajipamba kwa pete zake na ushanga, na kuwaendea wapenzi wake, akanisahau mimi. –Ni ujumbe wa Yawe.