Wafalme watakushugulikia, na malkia watakutengenezea chakula. Watainama mbele yako uso mpaka chini, na kulambula mavumbi ya miguu yako. Halafu utatambua kwamba mimi ni Yawe; wote wanaonitegemea hawatapata haya.
Wageni watakaoshikamana nami Yawe, kwa kunitumikia na kwa kupenda jina langu, na kuwa watumishi wangu, wote watakaoshika siku ya Sabato bila kuichafua, watu watakaofuata agano langu,
Watu wanaokaa katika inchi za mbali watakuja kusaidia kwa kulijenga hekalu langu mimi Yawe. Nanyi mutajua kwamba Yawe wa majeshi, ndiye aliyenituma kwenu. Haya yote yatatukia kama mukiitii sauti ya Yawe, Mungu wenu.