Biblia Todo Logo
အွန်လိုင်း သမ္မာကျမ်းစာ

- ကြော်ငြာတွေ -




Isaya 6:4 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

4 Sauti yao iliitikisa misingi ya milango ya hekalu, nalo likajaa moshi.

အခန်းကိုကြည့်ပါ။ ကော်ပီ




Isaya 6:4
12 ပူးပေါင်းရင်းမြစ်များ  

Waimbaji na wapiga baragumu wote pamoja walitoa sauti kwa pamoja na matoazi na vyombo vingine vya muziki, wakimusifu Yawe wakiimba: “Yeye ni muzuri. Wema wake unadumu milele.” Wakati ule nyumba ya Yawe ikajazwa na wingu.


Halafu dunia ikatetemeka na kutikisika, misingi ya milima ikayumbayumba na kutetemeka, kwa maana Mungu alikuwa amekasirika.


Kisha, lile wingu likafunika lile hema la mukutano na utukufu wa Yawe ukajaza hema.


Vilipokuwa vinakwenda, nilisikia sauti ya mabawa yao; sauti ya muvumo huo ilikuwa kama ile ya maji mengi, kama sauti ya ngurumo kutoka kwa Mungu wa majeshi, na kama kelele ya jeshi. Viliposimama, vilikunja mabawa yao.


Shindo la mabawa ya makerubi iliweza kusikilika hata kwenye kiwanja cha inje, kama sauti ya Yawe wa majeshi anaposema.


vyote vilipambwa kwa mbao tangu kwenye sakafu mpaka kwenye madirisha. Madirisha haya yangeweza kufunikwa.


Yule mutu akanipeleka mbele ya nyumba ya Yawe, kwa njia ya mulango wa kaskazini. Nilipoangalia, nikaona utukufu wa Yawe umeijaza nyumba ya Yawe. Hapo nikaanguka uso mpaka chini.


Nilimwona Yawe akisimama pembeni ya mazabahu, naye akaniamuru: Piga zile nguzo za hekalu mpaka misingi yake itikisike. Uvunje zile nguzo ziwaangukie watu juu ya vichwa. Wale watakaobaki nitawaua kwa upanga; hakuna hata mumoja wao atakayeponyoka, hakuna atakayetoroka.


Kisha hekalu la Mungu linalokuwa mbinguni likafunguliwa, na Sanduku la Agano lake likaonekana ndani yake. Halafu kukatokea umeme, makelele, ngurumo ya radi, tetemeko la inchi na mvua kubwa ya mawe.


Hekalu likajaa moshi kutokana na utukufu wa Mungu na uwezo wake. Na hakuna mutu aliyeweza kuingia ndani ya hekalu mpaka yale mapigo yaliyoletwa na wale wamalaika saba yalipotimizwa.


ကြှနျုပျတို့နောကျလိုကျပါ:

ကြော်ငြာတွေ


ကြော်ငြာတွေ