Yote yataachiwa ndege wa milima na nyama wengine wa pori. Ndege wakali watakaa humo wakati wa jua, na nyama wa pori watafanya makao humo wakati wa baridi.
Nitakutupa katika jangwa, wewe na samaki hao wote. Mwili wako utaangukia katika mbuga; wala hakuna atakayekuokota kusudi akuzike. Nimeutoa mwili wako ukuwe chakula cha nyama wakali na ndege.
Sasa, ewe mwanadamu, Bwana wetu Yawe anasema hivi: Uite ndege wote na nyama wote wa pori wakusanyike toka pande zote na kuja kukula karamu ya sadaka ya nyama ninayowatayarishia, ambayo itakuwa kubwa sana juu ya milima ya Israeli, ambako watakula nyama na kunywa damu.