Wale walionipiga, niliwaelekezea mugongo wangu, wale walioziongoa ndevu zangu, mashavu yangu. Sikuficha uso wangu wakati watu waliponitukana na kunitemea mate.
Yesu na wanafunzi wake walipokuwa katika njia, wakipanda kwenda Yerusalema, yeye akatangulia mbele yao. Wanafunzi walishikwa na hofu, nao watu waliowafuata waliogopa. Yesu akawatwaa tena wanafunzi wake kumi na wawili, na kuanza kusemezana nao juu ya mambo yatakayomupata.