Biblia Todo Logo
အွန်လိုင်း သမ္မာကျမ်းစာ

- ကြော်ငြာတွေ -




Isaya 51:6 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

6 Muinue macho, muangalie mbingu, kisha muangalie dunia kule chini. Mbingu zitatoweka kama moshi, dunia itachakaa kama nguo, na wakaaji wake watakufa kama vidudu. Lakini wokovu ninaouleta unadumu milele; ukombozi wangu hautakoma hata kidogo.

အခန်းကိုကြည့်ပါ။ ကော်ပီ




Isaya 51:6
27 ပူးပေါင်းရင်းမြစ်များ  

Lakini wema wa Yawe unadumu milele, kwa wale wote wanaomwabudu; na haki yake inadumu vizazi vyote,


Kila anachofanya kimejaa utukufu na heshima; haki yake inadumu milele.


Nitazitetemesha mbingu nayo inchi itatikisika katika misingi yake kwa sababu ya kasirani ya Yawe wa majeshi, siku ile ya hasira yangu kali.


Enyi watu wa Yerusalema, Yawe atawajalia usalama, atawaokoa na kuwapa hekima na maarifa. Akiba yenu kubwa ni kumwogopa Yawe.


Jeshi lote la anga litaharibika, anga zitakunjamana kama karatasi. Jeshi lake lote litanyauka, kama vile majani ya mizabibu au mitini yanavyonyauka.


Muinue macho yenu juu mbinguni! Ni nani aliyeziumba nyota hizo? Ni yule anayeziongoza kama jeshi lake, anayeijua hesabu yake yote, anayeziita kila moja kwa jina lake. Kwa sababu yeye ni mwenye nguvu nyingi, hakuna hata moja inayokosekana.


Lakini taifa la Israeli litaokolewa na Yawe, litapata wokovu wa milele. Halitapata haya wala kuzarauliwa milele.


Angalia Bwana wetu Yawe ananisaidia. Ni nani anayeweza kusema niko na kosa? Waadui zangu wote watachakaa kama nguo, nondo watawatafuna.


Maana watakuliwa na nondo kama vile nguo; vidudu watawakula kama wanavyokula nguo ya manyoya ya kondoo. Lakini ukombozi ninaouleta mimi utadumu milele; wokovu wangu hautakuwa na mwisho.


Milima inaweza kutoweka, vilima vinaweza kuondolewa, lakini rehema zangu kwako sitaziacha, agano langu la amani litaimarishwa. Ni Yawe anayekuhurumia anayesema hivyo.


Nitafanya kama nilivyofanya wakati wa Noa. Wakati ule niliapa kwamba sitaifunika tena dunia kwa mafuriko ya maji. Basi sasa ninaapa kwamba sitakukasirikia tena wala sitakukaripia tena.


Muda wa miaka saba mara makumi saba umewekwa kwa ajili ya watu wako na juu ya muji wako mutakatifu kwa kumaliza makosa, kukomesha zambi, kusamehe uovu, kuleta haki ya milele, kutia muhuri juu ya maono na unabii na kupakaa mafuta katika Pahali Patakatifu Sana.


Mbingu na dunia vitatoweka, lakini maneno yangu hayatabadilika hata kidogo.


“Kweli, kweli ninawaambia: anayesikia neno langu na kumwamini yule aliyenituma, anapata uzima wa milele. Yeye hatahukumiwa, lakini ameponyoka lufu na kupata uzima.


Mufanye angalisho kusudi wakati mutakapoangalia na kuona nyota, vitu vyote vya mbinguni, musivutwe kuviabudu na kuvitumikia. Vitu hivyo Yawe amewaachia watu wengine waviabudu.


Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe na Mungu Baba yetu, aliyetupenda na kwa neema yake akatufariji kwa milele na kutupatia tumaini njema,


Na alipokwisha kufanywa kuwa mukamilifu, akawaongoza watu wote wanaomutii wapate kuokolewa kwa milele.


Aliingia mara moja tu katika Pahali Patakatifu Sana. Naye hakupeleka mule sadaka ya damu ya mbuzi na ya ngombe, lakini alipeleka damu yake mwenyewe. Na kwa njia ile akatukomboa kwa milele.


Kwa sababu hii, Kristo ni mupatanishi wa agano jipya. Kwa njia ya kufa kwake aliwakomboa watu toka katika makosa waliyofanya chini ya uongozi wa agano la kwanza, kusudi wale walioalikwa na Mungu wapate kupokea urizi wa milele aliowaahidia.


Kisha nikaona kiti kikubwa cheupe cha kifalme pamoja na yule aliyeikaa juu yake. Dunia na mbingu vikatoweka mbele yake navyo havikuonekana tena.


ကြှနျုပျတို့နောကျလိုကျပါ:

ကြော်ငြာတွေ


ကြော်ငြာတွေ