9 Angalia Bwana wetu Yawe ananisaidia. Ni nani anayeweza kusema niko na kosa? Waadui zangu wote watachakaa kama nguo, nondo watawatafuna.
Nani atakayebishana nami? Niko tayari kunyamaza na kufa.
Nami ninaisha kama muti uliooza, kama nguo iliyokuliwa na nondo.
Wewe uliumba dunia tokea zamani, mbingu ni kazi ya mikono yako.
Usiniazibu tena; ninamalizika kwa mapigo yako.
Ninajua Mungu ni musaada wangu, Yawe anaimarisha maisha yangu.
Basi, usiogope, mimi nipo pamoja nawe. Usifazaike, mimi ni Mungu wako. Nitakuimarisha na kukusaidia; nitakulinda kwa mukono wangu wa ushindi.
Silaha zote zilizotengenezwa kwa kukuzuru wewe hazitafaa kwa kitu chochote. Mutu akikushitaki, utamushinda. Hiyo ndiyo haki niliyowapangia watumishi wangu. Hizo ndizo haki nilizowahakikishia. –Ni ujumbe wa Yawe.
Mali yenu imeoza, na nguo zenu zimekuliwa na nondo.