“Zaidi ya hayo, unajua vilevile yale Yoabu mwana wa Zeruya aliyonitendea, jinsi alivyowatendea majemadari wawili wa waaskari wa Israeli, Abeneri mwana wa Neri, na Amasa mwana wa Yeteri. Aliwaua wakati wa amani akitaka kulipiza kisasi kwa mauaji waliyofanya wakati wa vita. Aliwaua watu wasiokuwa na kosa, nami nikabeba lazima ya kifo cha watu wale kwa ajili ya vitendo vyake.