Isaya 49:22 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 200222 Bwana wetu Yawe anasema hivi: Nitasimika bendera kwa kuita mataifa; nitayaonyesha kitambulisho. Nayo yatawarudishia wana wenu wakiwabeba kwenye kifua, vilevile na wabinti zenu kwenye mabega. အခန်းကိုကြည့်ပါ။ |
Nitaweka kati yao kitambulisho cha uwezo wangu. Watakaookolewa kati yao nitawapeleka kwa watu wa mataifa kule Tarsisi, Puti, Ludi, inchi zenye wafundi wa kupiga upinde; watakwenda vilevile Tubali na Ugriki na katika visanga vya mbali ambapo watu hawajapata kusikia habari zangu wala kuuona utukufu wangu. Wale wajumbe wangu watautangaza utukufu wangu katika mataifa hayo.
Watawarudisha wandugu zenu wote kutoka katika mataifa yote kama matoleo yangu mimi Yawe. Watawaleta juu ya farasi, juu ya nyumbu, juu ya ngamia na ndani ya magari na juu ya vipoyi mpaka Yerusalema, kwenye mulima wangu mutakatifu. Watawaleta kama Waisraeli wanavyoleta sadaka ya unga katika chombo safi mpaka ndani ya nyumba yangu mimi Yawe.