Ni nani aliyemwita shujaa toka mashariki, mutu ambaye anapata ushindi popote anapoenda? Mimi ninayaweka mataifa katika mikono yake, naye anawaponda wafalme chini ya miguu yake! Upanga wake unawafanya kuwa kama mavumbi, kwa upinde wake anawapeperusha kama maganda.