20 Yawe ataniokoa. Nasi tutamusifu kwa nyimbo za vinubi siku zote za maisha yetu, katika nyumba ya Yawe.
Nitamwimbia Yawe maisha yangu yote; nitamusifu Mungu wangu muda wote nitakaoishi.
Yeye amenitegea sikio, hivyo nitamwomba muda wote wa maisha yangu.
Wimbo wa sifa wa Daudi. Nitakutukuza, ee Mungu wangu na mufalme wangu; nitalitukuza jina lako kwa milele na milele.
Nitakutukuza kila siku; nitalisifu jina lako kwa milele na milele.
Nitamusifu Yawe maisha yangu yote; nitamwimbia Mungu wangu muda wote nitakapoishi.
Mumusifu kwa ngoma na michezo, mumusifu kwa filimbi na kinanda!
Mushangilie kwa sababu ya Yawe, enyi watu wa haki! Watu wa usawa ndio wanaostahili kumusifu Mungu.
Mumusifu Yawe kwa zeze; mumwimbie kwa kinubi cha nyuzi kumi.
Halafu nitawafundisha wakosaji njia zako, nao wenye zambi watarudi kwako.
usafishe miguu katika damu ya waadui zako, nao imbwa wako wapate posho yao.”
Ee Mungu, maandamano yako ya ushindi yanaonekana; maandamano ya Mungu wangu, mufalme wangu, katika pahali patakatifu!
Mungu ndiye mwenye kuniokoa, nitamutegemea yeye, wala sitaogopa; Yawe ananijalia nguvu; yeye mwenyewe ndiye anayeniokoa.
Lakini mimi, kwa wimbo wa shukrani, nitakutolea sadaka, na kutimiza viapo vyangu. Yawe, ndiye anayeokoa.
Bwana, Yawe ndiye nguvu yangu, anaimarisha miguu yangu kama ya paa, ananiwezesha kupita juu katika milima. Kwa mwimbishaji: pamoja na ala za muziki wa nyuzi.