Naye akamwambia: “Kwa sababu umekataa kutii amri ya Yawe, basi, mara tu utakapoachana nami, simba atakuua.” Na kweli, mara tu alipoachana naye, akakutana na simba, akamwua.
Kwa hiyo mufalme akafurahi sana; akaamuru kwamba wamwondoe Danieli toka ndani ya pango. Basi wakamwondoa, naye hakuonekana na alama hata kidogo ya kidonda, kwa sababu alimutegemea Mungu wake.
Maana mimi nitakuwa kama simba kwa Efuraimu, kama simba mukali kwa watu wa Yuda. Mimi mwenyewe nitawararua na kuondoka, nitawakamata na hakuna atakayewaokoa.