Kisha mufalme wa Asuria akapeleka watu kutoka Babeli, Kuta, Awa, Hamati na Sefarwaimu na kuwaweka katika miji ya Samaria kwa pahali pa watu wa Israeli waliopelekwa katika uhamisho. Wakaitwaa miji hiyo na kukaa mule.
Hii ni juu ya Damasiki: Miji ya Hamati na Arpadi, imejaa wasiwasi kwa kufikiwa na habari mbaya; mioyo ya watu wake inayeyuka kwa hofu, imefazaika kama bahari isiyoweza kutulia.