Nilisema nitapanda muti wa ngazi na kuchuma shada za ngazi. Kwangu maziba yako ni kama shada za zabibu, harufu nzuri ya pumzi yako ni kama matunda ya mutofaa;
Katika siku zile Yesu akasema: “Ee Baba, Mwenyeji wa mbingu na dunia, ninakushukuru kwa maana mambo uliyoyaficha kwa watu wenye hekima na elimu, umeyafunua kwa wanaokuwa wadogo.
Halafu Yesu akamwambia: “Heri kwako, wewe Simoni mwana wa Yona, kwa maana hakuna mutu aliyekufunulia neno hili isipokuwa Baba yangu anayekuwa mbinguni.
Wajumbe wa Baraza Kubwa walishangaa sana kuona namna Petro na Yoane walivyosema bila woga na kujua kwamba walikuwa watu wasiojulikana na wasiokuwa na elimu. Wakatambua kwamba walikuwa pamoja na Yesu.