20 Lakini heri yenu ninyi: mutapanda mbegu zenu popote penye maji, ngombe na punda wenu watatembeatembea namna wanavyotaka.
Tupa chakula chako juu ya maji. Nyuma ya siku nyingi utakipata tena!
Siku ile watu waliosadiki mafundisho ya Petro, wakabatizwa. Na kadiri ya watu elfu tatu wakaongezeka katika kundi la wanafunzi.
Lakini wengi kati ya watu waliosikia mafundisho ya Petro na Yoane wakaamini. Kadiri ya watu elfu tano wakaongezeka katika kundi la waamini.
Hesabu ya watu waliomwamini Bwana, wanaume na wanawake, ilizidi kuongezeka sana.
Mimi nilipanda mbegu na Apolo alinyweshea maji, lakini Mungu ndiye aliyeiotesha.
Na tunda la haki linapandwa katika amani na wale wanaopenda amani.