Yoyakimu alikuwa na umri wa miaka makumi mbili na mitano alipoanza kutawala, akatawala kwa muda wa miaka kumi na mumoja akiwa kule Yerusalema. Alitenda maovu mbele ya Yawe, Mungu wake.
Yoyakini alikuwa na umri wa miaka minane alipoanza kutawala, alitawala kule Yerusalema kwa muda wa miezi mitatu na siku kumi. Alitenda maovu mbele ya Yawe.
Yawe anasema: Wanawake wa Sayuni wako na kiburi; wanatembea wakiinua kichwa juu, wakirembua macho yao kwa tamaa. Hatua zao ni za maringo, nao wanalilisha mikufu kwenye miguu yao.