Hiyo ni siku ya kuwaangamiza Wafilistini wote, kukomesha musaada uliobakia kutoka Tiro na Sidona. Maana Yawe anawaangamiza Wafilistini, watu waliobaki wa kisanga cha Kafutori.
Siku hiyo, nitapeleka wajumbe kwenda kuwatisha Waetiopia wanaojizania kuwa na usalama. Watatetemeka siku Misri itakapoangamia. Kweli! Kweli siku hiyo inakuja!