Yawe anasema hivi: Nitauazibu ulimwengu kwa uovu wake, waovu kwa sababu ya makosa yao. Nitakikomesha kiburi cha wenye majivuno, na kuporomosha mazarau ya watu wakali.
Maana Yawe anakuja kutoka kwake juu, kutoka makao yake huko mbinguni; kuwaazibu wakaaji wa dunia kwa uovu wao. Nayo dunia haitaficha tena wale waliouawa, lakini itaufichua umwagaji wa damu wote.
Mungu ni mwenye hekima na analeta maangamizi. Habadilishi masemi yake; lakini yuko tayari kuwaazibu watu waovu vilevile na wasaidizi wa watenda mabaya.
Hakutakuwa tena vifo vya watoto wachanga, wazee nao hawatakufa mbele ya wakati wao. Mutu wa miaka mia moja akikufa, amekufa akiwa kijana; na akikufa mbele ya miaka mia moja, ni kusema amelaaniwa.
Nitawalipiza maovu yao wayalipe vilevile maovu ya babu zao. –Ni Yawe anayesema hivyo.– Wao waliifukizia ubani miungu yao kwenye milima, wakanitukana mimi kule juu ya vilima. Nitawalipa sawa inavyostahili, watayalipa matendo yao ya zamani.