Miti ya shindano inafurahia kuanguka kwako, nayo mierezi ya Lebanoni pamoja inasema: Kwa vile sasa umeangushwa, hakuna mukata miti atakayekuja juu yetu!
Umewatuma watumishi wako kumuchekelea Bwana wenu; wewe umesema: Kwa magari yangu mengi ya vita, nimefika juu kwenye vichwa vya milima, mpaka kwenye vichwa vya milima ya Lebanoni. Nimeangusha mierezi yake mirefu, na misunobari mizurimizuri. Nimevifikia vichwa vyake na ndani ya pori zake kubwa.
Walitwaa miti ya mialo toka Basani wakakuchongea makasia; walikutengenezea mbao za kuikalia kwa miti ya misunobari ya kisanga cha Kipuro, na kuipamba kwa pembe ya tembo.