Isaya 18:6 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
6 Yote yataachiwa ndege wa milima na nyama wengine wa pori. Ndege wakali watakaa humo wakati wa jua, na nyama wa pori watafanya makao humo wakati wa baridi.
Lakini wewe umetupwa inje ya kaburi lako, kama mutoto wa kuchukiza aliyezaliwa mufu, kama maiti ambayo imekanyagwakanyagwa. Umelundikiwa maiti za waliouawa kwa upanga, waliotupwa ndani ya mashimo penye mawe.
(Ni Wakaldea, wala si Waasuria, waliowaacha nyama wa pori waushambulie muji wa Tiro. Wao ndio waliouzungushia muji huo minara ya kuushambulia, wakabomoa nyumba zake na kuufanya mabomoko.)
Hao watakufa kwa magonjwa makali, na hakuna atakayeomboleza juu yao wala kuwazika. Maiti zao zitabaki kama vile mboleo juu ya udongo. Wataangamia kwa vita na kwa njaa; na maiti zao zitakuwa chakula cha ndege na nyama wa pori.