Maji ya Dimoni yamejaa damu, lakini Mungu ataongeza musiba wa Dimoni. Hao wachache watakaobaki wazima na kukimbia kutoka Moabu, watapelekewa simba wa kuwaua.
Wavuvi watasimama kandokando ya bahari, na nafasi toka Engedi mpaka Eni-Eglaimu itakuwa ya kuanikia nyavu. Kutakuwa aina nyingi za samaki kama zinavyokuwa katika bahari ya Mediteranea.