Biblia Todo Logo
အွန်လိုင်း သမ္မာကျမ်းစာ

- ကြော်ငြာတွေ -




Isaya 14:12 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

12 Jinsi gani ulivyoporomoshwa toka mbinguni, wewe uliyekuwa nyota yenye kuangaza kwa mapambazuko. Jinsi gani ulivyoangushwa chini, wewe uliyeyashinda mataifa!

အခန်းကိုကြည့်ပါ။ ကော်ပီ




Isaya 14:12
18 ပူးပေါင်းရင်းမြစ်များ  

Nyota na vikundi vyake katika anga hazitaangaza; jua linapochomoza litakuwa giza, na mwezi hautatoa mwangaza wake.


Jeshi lote la anga litaharibika, anga zitakunjamana kama karatasi. Jeshi lake lote litanyauka, kama vile majani ya mizabibu au mitini yanavyonyauka.


Jinsi gani huo muji uliokuwa nyundo iliyoponda dunia nzima unavyoangushwa chini na kuvunjika! Babeli umekuwa pori tupu kati ya mataifa!


Ingawa Babeli ungepanda mpaka mbinguni, na kuziimarisha kuta zake ndefu, waangamizaji watakuja kutoka kwangu kwa kuuharibu. –Ni ujumbe wa Yawe.


Kwa hasira yake, Yawe amewaweka watu wa Sayuni katika giza. Ametupa toka mbinguni mpaka katika dunia utukufu wa Israeli. Kwa siku ya hasira yake, alilitupilia mbali hata hekalu lake.


Watakuimbia wimbo huu wa kuomboleza: Namna gani wewe muji wenye utukufu, umetoweka kutoka katika bahari! Ulikuwa na nguvu juu ya bahari, wewe pamoja na wakaaji wako, wewe uliyeletea woga juu ya wote!


Hata ukiruka juu kama tai, ukifanya makao yako kati ya nyota, mimi nitakushusha chini tu. –Ni ujumbe wa Yawe.


Naye Yesu akamwambia: “Nilimwona Shetani akianguka kama umeme toka mbinguni.


Vilevile tunaamini ujumbe uliotangazwa na manabii. Ninyi munafanya vema mukishikamana nao. Ujumbe huo ni kama taa inayoangaza pahali pa giza, mpaka wakati wa mapambazuko na wakati nyota ya asubui itakapoangazia mioyo yenu.


Kwa maana Mungu hakuwahurumia wale wamalaika waliofanya zambi, lakini aliwatupa katika jehenamu. Wao wanalindwa mule wakifungwa minyororo katika giza nzito wakingojea Siku ile ya hukumu.


akiwa na uwezo sawa ule uliopewa na Baba yangu. Na zaidi ya ile nitamupa nyota ya asubui.


“Mimi Yesu, nimemutuma malaika wangu kwa kuwashuhudia maneno haya yote katika kanisa. Mimi ni wa shina na wa uzao wa mufalme Daudi. Mimi ni nyota ya asubui.”


Kisha malaika wa tatu akapiga baragumu. Halafu nyota kubwa iliyowaka kama mwenge, ikaanguka toka mbinguni na kujitupa juu ya sehemu moja ya tatu ya mito na juu ya chemichemi.


Kisha malaika wa tano akapiga baragumu. Halafu nikaona nyota iliyokuwa imeshuka toka mbinguni, na kuanguka katika dunia. Nayo ikapewa ufunguo wa shimo ndefu la kuzimu.


ကြှနျုပျတို့နောကျလိုကျပါ:

ကြော်ငြာတွေ


ကြော်ငြာတွေ