Kwa nini munapiga kelele za shangwe, na muji wote umechangamuka na kujaa vigelegele? Watu wenu waliokufa hawakuuawa katika vita, wala hawakuuawa katika mapigano.
Kuzimu inawangoja kwa hamu kubwa, imepanua kinywa chake mpaka mwisho. Waheshimiwa pamoja na watu wengine wa Yerusalema wanaingia humo makundi kwa makundi, vilevile na wote wanaushangilia kwa furaha.
Maana watakuliwa na nondo kama vile nguo; vidudu watawakula kama wanavyokula nguo ya manyoya ya kondoo. Lakini ukombozi ninaouleta mimi utadumu milele; wokovu wangu hautakuwa na mwisho.
Kisha watakwenda kuziona maiti za wale walioniasi. Wadudu watakaowakula hawatakufa, na moto utakaowachoma hautazimika hata kidogo. Watakuwa chukizo kwa watu wote.