Isaya 1:11 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 200211 Yawe anasema hivi: Uwingi wa sadaka zenu ni kitu gani kwangu? Nimechoka na sadaka zenu za kondoo wenye kuteketezwa na mafuta ya nyama wenu wenye kunona. Sipendezwi na damu ya ngombe dume, wala ya wana-kondoo, wala ya beberu. အခန်းကိုကြည့်ပါ။ |
Lakini watu hawa wanafanya wanavyotaka: wananitolea sadaka ya ngombe na tena wanaua watu kwa kutambikia. Wananitolea sadaka ya mwana-kondoo na vilevile wanaua imbwa. Wananitolea sadaka ya unga na vilevile wanatolea damu ya nguruwe. Wanachoma ubani mbele yangu na kwenda kuabudu miungu ya uongo. Hao wamechagua kufuata njia zao wenyewe.