Lakini hawakukuwa waaminifu kwako. Wakakuasi, wakaacha sheria yako na kuwaua manabii waliowaonya kusudi wakurudilie wewe. Wakatenda zambi kubwa mbele yako.
Watu wangu wameangamia kwa kutonijua, maana wewe kuhani umekataa mafundisho. Nimekukataa kuwa kuhani wangu. Kwa maana umeisahau sheria ya Mungu wako, nami vilevile nitawasahau watoto wako.