Hosea 5:14 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
14 Maana mimi nitakuwa kama simba kwa Efuraimu, kama simba mukali kwa watu wa Yuda. Mimi mwenyewe nitawararua na kuondoka, nitawakamata na hakuna atakayewaokoa.
Waaskari wao wananguruma kama simba; wananguruma kama simba wakali ambao wamekamata nyama wao na kuwapeleka mbali ambapo hakuna anayeweza kuwanyanganya.
Halafu watasema: Tuende tumurudilie Yawe! Yeye mwenyewe ameturarua, lakini yeye mwenyewe atatuponyosha. Yeye mwenyewe ametuumiza, lakini yeye mwenyewe atatunza vidonda.
Ngombe wenu watachinjwa mbele ya macho yenu lakini hamutaonja hata kipande cha nyama yao. Punda wenu watatwaliwa kwa nguvu mbele ya macho yenu wala hamutarudishiwa. Kondoo wenu watapewa waadui zenu, na hakuna mutu atakayeweza kuwasaidia.
Muone kwamba mimi ni Mungu na wala hakuna mwingine isipokuwa mimi. Mimi ninaua na kuweka uzima, ninaumiza na kuponya, na hakuna anayeweza kumwokoa yeyote toka katika mikono yangu.