Kwa hiyo, kama vile moto unavyoteketeza nyasi, kama vile majani yanavyotoweka ndani ya moto, ndivyo mizizi yao itakavyooza, na maua yao yatakavyopeperushwa juu kama mavumbi. Maana wameacha sheria ya Yawe wa majeshi, wamezarau neno la yule Mutakatifu wa Israeli.
Maana watakuliwa na nondo kama vile nguo; vidudu watawakula kama wanavyokula nguo ya manyoya ya kondoo. Lakini ukombozi ninaouleta mimi utadumu milele; wokovu wangu hautakuwa na mwisho.