Ee Yawe, tumaini la Waisraeli, wote wanaokukataa wafezeheshwe. Wanaokuacha wewe watatoweka, kama majina yaliyoandikwa chini katika mavumbi, kwa maana wamekuacha wewe Yawe, unayekuwa chemichemi ya maji ya uzima.
Hata kama Efuraimu atastawi kama nyasi, mimi Yawe nitavumisha upepo mukali wa mashariki, upepo utakaotokea kule katika jangwa, nao utakausha visima vyake, chemichemi zake zitakauka. Vitu vyake vyote vya bei kali vitaharibiwa.