Hosea 13:8 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
8 Nitawarukia kama dubu aliyenyanganywa watoto wake. Nitawararua vifua vyenu na kuwakula palepale kama simba; nitawararua vipandevipande kama nyama wa pori.
Zaidi ya hayo, Husayi akamwambia: “Wewe unajua kwamba baba yako na watu wake ni mashujaa na kwamba wamekasirikishwa kama dubu dike aliyenyanganywa watoto wake katika mbuga. Zaidi ya hayo, unajua kwamba baba yako ni bingwa wa vita. Yeye hatakaa usiku kucha pamoja na watu wake.
Waaskari wao wananguruma kama simba; wananguruma kama simba wakali ambao wamekamata nyama wao na kuwapeleka mbali ambapo hakuna anayeweza kuwanyanganya.
Maana mimi nitakuwa kama simba kwa Efuraimu, kama simba mukali kwa watu wa Yuda. Mimi mwenyewe nitawararua na kuondoka, nitawakamata na hakuna atakayewaokoa.