Kutoka jangwa la Sini, Waisraeli wote pamoja wakasafiri hatua kwa hatua kama vile Yawe alivyoamuru. Watu wakapiga kambi kule Refidimu. Lakini kule hakukukuwa maji ya kunywa.
Kama vile ngombe wanavyopelekwa kwa kulishwa katika bonde, ndivyo Roho wa Mungu alivyowapumzisha watu wake. Ndivyo, ee Mungu ulivyowaongoza watu wako, nawe ukajipatia jina tukufu.
Yawe wa majeshi anasema hivi: Ukifuata njia zangu na kushika maagizo niliyokupa, basi, utaisimamia nyumba yangu na viwanja vyake. Nami nitakuwezesha kuingia katika utumishi wangu kama hawa wanaosimama mbele yangu.