Kutoka jangwa la Sini, Waisraeli wote pamoja wakasafiri hatua kwa hatua kama vile Yawe alivyoamuru. Watu wakapiga kambi kule Refidimu. Lakini kule hakukukuwa maji ya kunywa.
Hawatasikia tena njaa wala kuwa na kiu. Upepo wenye kuunguza wala jua havitawachoma, mimi niliyewahurumia nitawaongoza na kuwapeleka kwenye chemichemi za maji.
Ikiwa ni siku mbili, mwezi, mwaka au zaidi, muda wote wingu hilo lilipokuwa juu ya hema, Waisraeli hawakuhama; lakini lilipoinuliwa, nao vilevile walihama.