Hiyo ndiyo sheria inayoelekea munaziri anayeahidi kwa kiapo. Sadaka yake kwa Yawe ilingane na kiapo chake, zaidi ya kitu chochote kingine anachoweza kutoa; atafanya kulingana na kiapo alichoweka, kadiri ya sheria ya kujitakasa kwake.
Siku zote za kiapo chake cha kujitenga, hatanyoa nywele zake. Mpaka muda wa kiapo chake cha kujitakasa kwa Yawe utakapomalizika, atakuwa mutakatifu, ataacha nywele zake zikuwe ndefu.