Haruni alipomaliza kutolea sadaka zote: sadaka kwa ajili ya zambi, sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, akawainulia watu mikono, akawabariki, kisha akashuka chini.
Hiyo ndiyo sheria inayoelekea munaziri anayeahidi kwa kiapo. Sadaka yake kwa Yawe ilingane na kiapo chake, zaidi ya kitu chochote kingine anachoweza kutoa; atafanya kulingana na kiapo alichoweka, kadiri ya sheria ya kujitakasa kwake.
Nao makuhani wa ukoo wa Lawi sharti wakuwe pale. Yawe, Mungu wenu, aliwachagua wamutumikie na kubariki kwa jina lake. Wao vilevile ndio wenye mamlaka ya kuamua magomvi na maneno juu ya kuumizana.