na kujitakasa kwa Yawe kwa siku zake za kujitenga. Hizo siku za kwanza hazitahesabiwa kwa sababu nywele zake zilizokuwa zimetakaswa zimechafuka. Atatoa mwana-kondoo dume wa mwaka mumoja kuwa sadaka ya kosa.
Halafu kesho yake Paulo akaenda na wale watu wane, na akajitakasa pamoja nao. Kisha akaingia ndani ya hekalu na kutangaza wakati siku za utakaso zitakapotimia, na sadaka itakayotolewa kama malipo kwa ajili ya kila mumoja wao.
Zile siku saba zilipokaribia kutimia, Wayuda wamoja waliotoka katika jimbo la Azia wakamwona Paulo ndani ya hekalu. Wao wakashawishi watu wote waliokusanyika, wakamukamata