Hivyo siku zote Waisraeli watatwaa sehemu hizo kutoka katika sadaka zao za amani wanazonitolea mimi Yawe na kumupa Haruni na wana wake. Hiyo ni sadaka yao kwa Yawe.
Mutaikula katika Pahali Patakatifu kwa sababu hiyo ni haki yako na wazao wako kutoka katika sadaka Yawe anazotolewa kwa moto. Hivi ndivyo nilivyoamuriwa.