Ukoo wa Gersoni, kulingana na jamaa zake ulipewa miji kumi na mitatu katika kabila la Isakari, na katika kabila la Nafutali na katika kabila la Manase katika Basani.
Hii ndiyo iliyokuwa hesabu ya watu wa jamaa za wana wa Gersoni wote waliotumika katika hema la mukutano, ambao Musa na Haruni waliwahesabu kama vile Yawe alivyowaamuru.