Hii ndiyo hesabu ya vifaa vilivyotumika katika kujenga hema la kuchunga vile vibao vya agano. Hesabu hii ilitayarishwa na Walawi kwa amri ya Musa, chini ya uongozi wa Itamari mwana wa kuhani Haruni.
Haruni na wana wake makuhani ndio watakaoamrisha kazi zote za Wagersoni juu ya vitu watakavyobeba na kazi watakazofanya. Utawapangia vitu vyote vile ambavyo wanapaswa kubeba.
Hii ndiyo itakayokuwa kazi ya wana wa ukoo wa Merari katika utumishi wao wote ndani ya hema la mukutano, chini ya uongozi wa Itamari mwana wa kuhani Haruni.