2 Uhesabu watu wa ukoo wa Kohati, toka katika ukoo za Lawi, kufuatana na jamaa zao na ukoo zao;
Wana wa Kohati kwa kufuata jamaa zao: Amuramu, Isihari, Hebroni na Uzieli.
Jamaa za Waamuramu, Waisari, Wahebroni na Wauzieli zilitokana na Kohati; hizi ndizo zilizokuwa jamaa za Wakohati.
Yawe akamwambia Musa na Haruni:
utahesabu wanaume wote wenye umri kati ya miaka makumi tatu na makumi tano wanaofaa kujiunga na kazi ya hema la mukutano.