Hesabu 4:11 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
11 Halafu watatandaza kitambaa cha rangi ya samawi juu ya mazabahu ya zahabu na kuifunika kwa ngozi laini ya mbuzi. Halafu wataingiza miti yake ya kuibebea.
Watatwaa vyombo vyote vinavyotumika katika Pahali Patakatifu, watavifunga kwa kitambaa cha rangi ya samawi na kuvifunika kwa ngozi laini ya mbuzi, kisha wataviweka juu ya miti yake ya kubebea.
Juu yake wataweka kifuniko cha ngozi laini ya mbuzi, kisha watatandaza juu yake kitambaa cha rangi ya samawi tupu. Halafu wataingiza miti ya kulibebea sanduku hilo.
Kisha malaika mwingine akakuja kusimama karibu na mazabahu. Alikuwa akishika chetezo cha zahabu. Naye akapewa ubani mwingi kusudi autoe sadaka pamoja na maombi ya watu wote wa Mungu juu ya mazabahu ya zahabu iliyokuwa mbele ya kiti cha kifalme.