4 Katika sikukuu ya ukumbusho urizi wao utahesabiwa pamoja na ule wa kabila watakamoolewa na hivyo kabila letu halitapata urizi huo tena.
Amenituma kutangaza mwaka wake wa neema, na siku ya Mungu wetu ya kulipiza kisasi kusudi niwafariji wote wanaoomboleza.
Musiuzishe mashamba kabisa, maana hiyo ni mali yangu na ninyi ni wageni na wasafiri katika inchi yangu.
Mutahesabu miaka saba mara saba na jumla yake ni miaka makumi ine na tisa.
Lakini wao wakiolewa na Waisraeli wa makabila mengine, urizi wao utatoka kwetu na kuwaendea watu wa kabila watakamoolewa; kwa hiyo urizi wetu sisi utapunguka.
Basi, Musa akawapa Waisraeli agizo lile kutoka kwa Yawe, akawaambia: Watu wa ukoo wa kabila la Yosefu wamesema ukweli.