“Tulipoitwaa inchi hiyo, nikawapa makabila ya Rubeni na Gadi eneo la kuanzia upande wa kaskazini wa Aroeri karibu na Arnoni na nusu ya eneo la milima ya Gileadi, pamoja na miji yake.
Watu wa kabila la Manase ambaye alikuwa muzaliwa wa kwanza wa Yosefu, vilevile walipewa eneo lao kwa kura. Makiri, muzaliwa wa kwanza wa Manase baba ya Gileadi, alikwisha kupewa kwa kura miji ya Gileadi na Basani, maana alikuwa hodari katika vita.